MAN CITY HOI KWA LIVERPOOL YALIZWA TENA NYUMBANI NA KUTUPWA NJE MABINGWA ULAYA

Man City 1-2 Liverpool (Agg 1-5): Salah and Firmino send Reds through
Ni wiki moja ya machungu kwa kocha Pep Guadiola baada ya kutupwa nje katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa kipigo cha bao 2-1 walichokipata dhidi ya Liverpool katika uwanja wao wa nyumbani.

Manchester City ambayo wachambuzi wengi wa soka waliiona kama ingeweza kubadilisha matokeo ya bao 3-0 walipofungwa wiki iliyopita lakini hali ilikua tofauti hasa baada ya kuanza kipindi cha pili.

Gabriel Jesus aliipatia Manchester City bao la kuongoza dakika ya 2 tu ya mchezo na kwajinsi walivyocheza vyema ilionekana kabisa mabao mengine yangepatikana.

Mohamed salah na roberto Firminho waliifungia Liverpool mabao kipindi cha pili baada ya uzembe wa mabeki wa Manchester City hivyo kufanya mchezo huo kumalizika kwa ushindi kwa Liverpool ambao umewafanya kutinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa bao 5-1

No comments

Powered by Blogger.