KUSUKA AU KUNYOA KWA GUADIOLA LEO MABINGWA ULAYA, BARCELONA MTEREMKO KWA ROMA
Mechi za marudiano katika hatua ya robo fainali ligi ya mabingwa Ulaya zitachezwa leo na kesho kupata timu nne zitakazotinga hatua ya nusu fainali.
Macho na msikio ya wapendasoka duniani yatakua katika dimba la Etihadi jijini Manchester ambapo Vinara wa ligi kuu ya England Manchester City wataialika Liverpool katika pambano linaloonekana litavuta hisia ndani na nje ya Uwanja.
Manchester city chini ya Pep Guadiola wao watakua na jukumu moja tu la kuhakikisha wanafunga mabao mengi iwezekanavyo bila kuruhusu kufungwa bao lolote baada ya mechi ya awali kuambulia kichapo cha bao 3-0 hivyo ili wavuke hatua hii wanahitaji kushinda si chini ya bao 4-0.
City Itaingia katika mchezo wa leo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza michezo miwili mfululizo iliyopita dhidi ya Liverpool ugenini na ule wa juzi dhidi ya Manchester United katika ligi kuu ya England.
jijini Roma wenyeji AS Roma watakua nyumbani kuialika Barcelona katika mchezo ambao unaonekana kuwa mwepesi kwa Barcelona kutokana na Ushindi walioupata katika pambano la awali pale Nou Camp wa goli 4-1 hivyo kuhitaji sare au hata wakifungwa basi yasizidi mabao 2-0.
Mechi zote hizi zinatarajiwa kuanza saa 4 kasorobo za usiku kwa sasa za afraika mashariki
No comments