AKIFUNGA KESHO TU, RONALDO ATAJIWEKEA REKODI NYINGINE YA KIPEKEE KATIKA SOKA
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji anashikilia rekodi nyingi zaidi duniani ambazo hakuna mchezaji aliyewahi kuzifikia. Ronaldo amekua akiweka rekodi mpya kila anapofunga na hili linaendelea kujidhihirisha katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu.
Wiki iliyopita Baada ya Ronaldo kufunga mabao mawili katika ushindi wa bao 3-0 walioupata Real Madrid dhidi ya Juventus amefikisha idadi ya mabao 14 ambayo ameshafunga msimu na kumweka katika orodha ya wachezaji watatu waliofikia idadi hiyo katika msimu mmoja Ronaldo anahitaji kufunga bao moja tu katika mechi zilizobaki kwenye michuano hiyo ukiwemo mchezo wa kesho Jumatano ambapo Real Madrid watakua nyumbani kuwaalika Juventus ili kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutawala top 3 ya wafungaji bora wa msimu katika michuano hiyo.
Ikumbukwe Ronaldo ndiye anayeongoza Kwa kuwa mchezaji pekee aliyefunga mabao mengi katika msimu mmoja wa Ligi ya mabingwa Ulaya akishafanya hivyo msimu wa mwaka 2013/2014 alilofunga mabao 17 kisha akafisha mabao 16 msimu uliopita kwahiyo namba 1 na namba 2 inashikwa na yeye mwenyewe wakati namba 3 inashikwa na wachezaji watatu akiwemo yeye Ronaldo, Lionel Messi wa Barcelona na mchezaji wa zamani wa AC Milan Jose Altafini aliyetamba miaka ya 1962/1963.
Msimamo Ulivyo Hivi sasa kwa wafungaji bora katika msimu mmoja
- Cristiano Ronaldo - (2013/2014) - 17 Goals
- Cristiano Ronaldo (2015/2016) - 16 Goals
- Cristiano Ronaldo (2017/2018) Lionel Messi (2011/2012) Jose Altafini (1962/1963) - 14 Goals
Kama Real Madrid watavuka na kuingia hatua ya nusu fainali na pengine fainali tunaweza kushuhudia Ronaldo akivunja rekodi ya mabao 17 aliyoiweka mwenyewe.
Ronaldo ndiye mfungaji bora wa muda wote wa michuano hiyo akiwa tayari amefunga mabao 119
No comments