BAYERN MUNICH YATAKATA UGENINI MABINGWA ULAYA
Wababe wa Manchester United klabu ya Sevila imeanza vibaya hatua ya Robo fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kufungwa bao 2-1 na BAYERN MUNICH
Mpaka Mapumziko timu hizo zilikua sare ya bao 1-1 baada ya Pablo Sarabia kuifungia Sevilla bao la kwanza dakika ya 30 ya mchezo lakini Jesus Navas akaisawazishia Bayern Munich bao hilo akijifunga na kufanya mpira kwenda mapumziko timu hizo zikitoshana nguvu ya bao 1-1.
Kipindi cha Pili Goli pekee la kipindi hicho likifungwa na Thiago Alcantara na kuwafanya Bayern kupata ahuweni kubwa kuelekea kwenye mechi ya marudiano itakayochezwa Alianz Arena wiki Ijayo.
No comments