RONALDO AWAFANYIA KITU MBAYA JUVENTUS KWAO LIGI YA MABINGWA ULAYA


Mchezaji bora wa Dunia na Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amefunga mabao mawili Katika ushindi wa bao 3-0 walioupata Real Madrid dhidi ya Juventus.



Mechi hiyo ya kwanza ya hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya Ilicheza jijini Turin huku Juventus wakiwa ndiyo Wenyeji.

Dakika 3 tu zilimtosha Ronaldo kuifunga Real Madrid bao la Kuongoza baada ya kuunganisha mpira wa krosi ya chini chini ya Isco bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko

Kipindi cha pili Ronaldo aliongeza bao la pili kwa kuunganisha krosi ya beki wa Real Madrid Dan Calvajal akifunga kwa tik taka na mpira kujaa wavuni goli lililoshangiliwa uwanja mzima wakiwemo mashabiki wa Juventus likiwa moja ya magoli bora kabisa.

Dakika chache baada ya goli Hilo Ronaldo alimtengeneze Marcelo ambaye naye akafunga bao lake ambalo lilikua la tatu Kwa Real Madrid kuwafanya Juventus kuwa na mlima mrefu wa kuupanda katika mechi ya marudiano wiki Ijayo.
Juventus walipata pigo pia baada ya mshambuliaji wake Paulo Dyabala kuonyeshwa kadi Nyekundu ambayo itamfanya kuukosa mchezo wa marudiano wiki Ijayo.

Ronaldo Kwa magoli mawili aliyowafunga Juventus amefikisha magoli 25 katika mechi 14 akiwa na Real Madrid na timu yake ya Taifa lakini pia amekua mchezaji wa kwanza kufunga magoli katika mechi 10 mfululizo za ligi ya mabingwa Ulaya akiwa amefikisha pia magoli 14 na assist 2 msimu huu.

No comments

Powered by Blogger.