ARSENAL YAZINDUKA "JIONI" NA KUISHUSHIA KICHAPO STOKE CITY 


Iliwachukua Arsenal dakika 75 kuweza kupata bao la kwanza katika ushindi wa bao 3-0 walioupata kwenye ligi kuu ya England dhidi ya Stoke City Leo.

Pierre-Emenick Aubameyang alifunga bao Hilo la kwanza baada ya beki wa Stoke City Bruno Martins-Indi kumfanyia madhambi Mesuit Ozil na Aubameyang kufunga bao hilo.

Dakika 10 baadae Aubameyang aliiwezesha Arsenal kufunga bao la pili baada ya KAZI nzuri ya kazi nzuri ya Mesuit Ozil na kuendelea kufufua  matumaini Kwa Arsenal ambao kipindi cha kwanza hawakucheza vizuri sana.

Arsenal  walipata penati ya pili katika mchezo huo na ilifungwa kiufundi na Alexandre Lacazette baada ya Badou Ndiaye kumsukuma Lacazete.

Ushindi huo unawafanya Arsenal kufikisha pointi 51 katika nafasi ya 6 huku Kwa Stoke ni msiba kwani wanabaki na point zao 27 katika nafasi ya 19.

1 comment:

Powered by Blogger.