PASAKA YAWA CHUNGU KWA CHELSEA, YALIZWA NA SPURS DARAJANI


Historia inaonyesha kabla ya mechi ya Leo baina ya Chelsea na Tottenham Hotspur Imepita miaka 28 tangu Tottenham Hotspur walipoifunga Chelsea Kwa Mara ya mwisho kwenye ligi kuu ya England katika uwanja wa Stamford Bridge.


Tottenham Hotspur ya sasa chini ya kocha Mauricio Pochettino imeweza kuvunja mwiko huo na kuibuka na ushindi wa bao 3-1 katika mchezo uliopigwa jioni hii kwenye dimba la Stamford Bridge

Alvaro Morata alifunga bao lake la kwanza katika ligi tangu Boxing day akiipatia Chelsea bao la Kuongoza akiunganisha mpira wa krosi ya Victor Moses dakika ya 30 lakini dakika moja kabla ya mapumziko Kiungo  wa Spurs Christian Eriksen aliipatia Spurs bao la kusawazisha kwa shuti Kali la mita zaidi ya 25 ambapo kipa wa Chelsea Caballero alikua hana la kufanya na mchezo huo kwenda mapumziko ukiwa sare ya bao 1-1.


Kipindi cha Pili Tottenham waliamka na kuongeza mashambulizi yaliyozaa bao la pili na la tatu yote yakifungwa na Delle Alli na kufanya mchezo huo kumalizika Kwa ushindi huo wa bao 3-1 walioupata Tottenham Hotspur.

Matokeo hayo yanaifanya Chelsea sasa kusubiri miujiza kuweza kucheza katika ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu ujao kwani wanaendelea kubaki na point zao 56 katika nafasi ya 5 wakati Tottenham wao wanafikisha pointi 64 katika nafasi ya 4.

No comments

Powered by Blogger.