ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE: ARSENAL NA ATLETICO MADRID ZAKWEPANA
Arsenal na Atletico
Madrid zimepangwa katika mechi tofauti kwenye droo ya hatua ya Robo fainali ya
michuano ya Kombe la Europa league ambayo ni ya pili kwa ukubwa katika hatua ya
klabu barani Ulaya.
Baada ya kuitoa AC Milan sasa Arsenal itacheza dhidi ya CSKA Moscow, Atletico Madrid yenyewe ikipangwa kucheza dhidi ya Sporting lisbon ya Ureno, RB Leipzig ikipangwa kucheza dhidi ya Olympique Marseille wakati Lazio kutoka Italia ikipangwa kucheza dhidi ya FC Salzburg ya Austria.
Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa Alhamisi ya April 6 na marudiano ni baada ya wiki moja yani April 12 mwaka huu 2018.
No comments