MAN CITY YAKABIDHIWA LIVERPOOL, MADRID NA JUVENTUS ROBO FAINALI MABINGWA ULAYA

Liverpool face Man City in Champions League quarter-final and more

Droo ya ligi ya mabingwa Barani Ulaya hatua ya Robo fainali imepangwa muda mchache uliopita ambazo timu 8 zimepangwa kukutana katika hatua hii 

Mabingwa watetezi Real madrid baada ya kuwaondoa PSG sasa wamepangwa kukutana na Mabingwa wa Italia klabu ya Juventus ikiwa ni kama marudio ya fainali iliyopita ya michuano hiyo ambapo juventus walikubaki kichapo na Real madrid kutawazwa mabingwa kwa mara ya pili mfululizo.

Pigo limeenda kwa klabu za England ambapo katika hatua ya nusu fainali ni klabu moja tu itakayoweza kuvuka na kuingia hatua hiyo kwani Manchester City imepangwa kucheza dhidi ya Liverpool katika hatua hii ya Robo fainali.

Barcelona baada ya kuitupa nje Chelsea safari hii wamepangwa kucheza na AS Roma toka Italia klabu ambayo imefuzu kwa faida ya bao la ugenini katika hatua iliyopita.

Sevilla ambao Jumanne wiki hii walizua gumzo duniani walipoiondosha Manchester United safari hii wamepangwa kukutana na vigogo wa ligi kuu ya Ujerumani klabu ya Bayern Munich.

mechi za hatua hii ya Robo fainali zimepangwa kuchezwa Aprili 3 na 4 mwaka huu huku marudiano ikiwa ni wiki moja baadae yani Aprili 10 na 11 mwaka huu 2018. 

No comments

Powered by Blogger.