ARSENAL MMESIKIA? CHELSEA WANAMTAKA AARON RAMSEY

The Welsh midfielder's Arsenal contract expires in June 2019 and a renewal is not close 

Chelsea wamegonga hodi kwa majirani zao Arsenal wakitaka kumsajili kiungo wa kimataifa wa Wales Aaron Ramsey ambaye amebakiza mwaka mmoja kumaliza mkataba wake na Arsenal.

habari kutoka vyanzo mbalimbali vya habari barani Ulaya ambazo www.wapendasoka.com tumezipata zinaeleza mazungumzo kati ya Arsenal na mchezaji huyo kuhusu kuongeza mkataba yamekwama na ndicho kilichowapa nguvu chelsea kuweza kumtolea macho.


Ramsey mwenye uwezo mkubwa wa kufunga anataka kusaini mkataba mpya tu endapo Arsenal watakubali kumwongezea mshahara akiwa napata paundi 110,000 kwa wiki katika mkataba wake wa sasa na pengine hii imechagizwa na kuona Mesuit Ozil ameongezewa mshahara mpaka kufikia paundi 300,000 kwa wiki.


mazungumzo ya mkataba mpya ndani ya Arsenal yanaonekana kukwama wakati huu ambapo Jack Wilshere, Aaron Ramsey, Danny Welbeck, Petr Cech, David Ospina na nacho Monreal wote hawa mikataba yao inaisha mwakani

No comments

Powered by Blogger.