MARCOS ROJO ANOGEWA MAN UNITED, KAONGEZA MKATABA NA KUIKACHA PSG

Marcos Rojo has signed a new three-and-a-half-year deal with Manchester United on Friday
Uvumi wa matajiri wa Ufaransa klabu ya PSG kutaka kumsajili Beki wa kimataifa wa Argentina anayeichezea Manchester United umezikwa rasmi leo baada ya beki huyo kusaini mkataba mpya wa kuichezea Manchester United.


Marcos Rojo amesaini leo Ijumaa mkataba mpya wa miaka mitatu na nusu ambao utamweka Old Trafford mpaka mwaka 2022 kukiwa pia na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja utakapomalizika na mkataba wake wa sasa ulikua unamalizika msimu ujao 

Taarifa zilikua zikimuhusisha Marcos Rojo na uhamisho wake kuelekea PSG huku ada ya paundi milioni 30 ikitajwa kama pesa iliyotengwa kumnyakua.

Nyongeza ya zaidi ya paundi 70,000 anazolipwa hivi sasa inatajwa kuongezeka katika mkataba wake mchezaji huyo mwenye miaka 27 hivi sasa ambaye amekua akisumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara

No comments

Powered by Blogger.