NGORONGORO YAENDELEA KUTOA DOZI

Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Msumbiji katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa.

Juzi Jumatatu timu hiyo inayofundishwa na kocha Ammy Ninje iliibuka pia na ushindi wa bao moja dhidi ya Morocco katika mchezo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Uhuru.

Vijana hao wameonyesha uwezo mkubwa katika michezo yote miwili kitu ambacho kinatoa matumaini kwa timu ya Taifa kwa siku za baadae.

Msumbiji walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 13 kupitia kwa Lionel Victor kabla ya Abdul Seleman kusawazisha dakika ya 35.

Winga Said Musa ambaye anachezea Yanga ndiye alifunga bao la ushindi dakika ya 71 akiihakikishia Ngorongoro kubaki na alama zote tatu.

Kikosi hicho kinajiandaa na michuano ya vijana ya Afrika utakayofanyika baadae mwaka huu.

No comments

Powered by Blogger.