SINGIDA UNITED: YAKANUSHWA KUFUNGIWA KWA DANNY LYANGA
Uongozi wa klabu ya Singida United
kupitia kwa Mkurugenzi mkuu Festo Sanga umekanusha taarifa za kufungiwa
kwa mshambuliaji wao Daniel Lyanga na shirikisho la soka Duniani FIFA
kwa madai ya kusaini mkataba na timu mbili.
Sanga amesema anashangaa kusikia
taarifa hizo bila uongozi wao kuulizwa ni nini chanzo kilichomfanya Lyanga
asiweze kucheza katika michuano ya ligi kuu na Azam Sports Federation Cup toka
asajiliwe katika dirisha dogo Disemba mwaka jana.
Sanga amesema ukweli wa jambo hilo ni kuwa Lyanga alisajiliwa
katika dakika za mwisho kabisa Kabla ya dirisha la usajili kufungwa kwa
makubaliano na klabu ya Fanja ya Oman lakini cheti cha uhamisho (ITC)' ndicho
kilichochelewa.
Lyanga alipewa barua ya kuachwa na klabu yakye
ya Fanja wakati wakitaka kumsajil, taarifa kuwa Danny lyanga amefungiwa sio kweli.
Asubuhi ya leo kumezuka
taarifa ya kuwa Daniel Lyanga amefungiwa miezi sita na FIFA kwa kusaini mkataba
na timu mbili tofauti Fanja FC ya Oman na Singida United ya Tanzania.
No comments