HATIMAYE PETR CECH AOKOA PENATI.

Jumapili ya leo imekua ya furaha kwa mlinda mlango wa Arsenal, Petr Cech  ambaye hatimaye amefanikiwa kuokoa mkwaju wa penalt kwa timu yake hiyo kwa mara ya kwanza tangu ajiunge nayo.

Cech ni kati ya magolikipa wenye uwezo mkubwa langoni akifanya kazi hiyo kwa muda mrefu katika klabu ya Chelsea na sasa Arsenal lakini changamoto kubwa kwake imekua ni kukosa ujanja linapokuja suala la penati.

Kabla ya kufanikiwa kuokoa penati leo katika mchezo dhidi ya Watford, Cech alikwisha shuhudia mipira 15 ya penati ikijaa langoni kwake huku akishindwa kuokoa mchomo wowote. Katika penati 15 alizofungwa, 12 alikwenda uelekeo tofauti na mpira hali inayoashiria udhaifu kwa mlinda mlango huyo.

Hatimaye jinamizi hilo limemtoka leo hii baada ya kuokoa mkwaju wa Troy Deeney uliopatikana baada ya Ainsley Maintland-Niles kumwabgusha Roberto Pereyra katika eneo la hatari kwenye mchezo ulioshuhudia Arsenal wakiibuka na ushindi wa 3-0.

No comments

Powered by Blogger.