KATWILA: TULICHEZA SISI TUMEFUNGWA SISI
Kocha mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema wachezaji wake walionyesha kandanda safi katika mchezo waliokubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Maafande wa Tanzania Prisons katika dimba la Sokoine.
Mtibwa imekuwa ikipata vipigo vya mfululizo tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi wakipata pointi moja katika michezo mitano.
Katwila alisema walimiliki mchezo huo muda mrefu lakini makosa waliyofanya yaliwagharimu na kujikuta wakipoteza mchezo huo.
"Tulicheza vizuri, tulitawala sehemu kubwa ya mchezo lakini wenzetu walipata nafasi mbili wakazitumia na kupata pointi tatu.
"Tunarudi nyumbani kujipanga kwa ajili ya michezo mingine na tutayafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza," alisema Katwila.
Mtibwa walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa kwa mkwaju wa penati na mshambuliji Stamili Mbonde kabla ya Salum Kimenya kusawazisha na kufunga bao la ushindi.
Matokeo ya mechi nyingine za ligi zilizochewa leo
Tanzania Prisons 2-1 Mtibwa
Singida United 0-0 Ndanda FC
Ruvu Shooting 2-2 Mbeya City
Majimaji 0-0 Lipuli FC

No comments