KUIONA SIMBA "YA KIMATAIFA" JUMAPILI NI BUKU 5 TU
Vinara wa ligi kuu Soka Tanzania bara Wekundu wa
Msimbazi Simba Jumapili ya wiki hii wanaerejea katika anga za kimataifa
watakapoikaribisha Gendarmerie Nationale ya Djibouti katika mchezo wa hatua ya
kwanza ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam Majira ya Saa 10 jioni huku Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee
Ally Hassan Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
Viingilio katika mchezo huo vitakuwa VIP A Tsh
30,000 wakati VIP B itakua ni TSh 20,000, Jukwaa la rangi ya chungwa
(Orange) utakua ni 10,000 na mzunguko ambao viti vyake ni vya kijani kiingilio
itakuwa buku tano tu (Tsh 5,000)
Akiongea na waandishi wa Habari Msemaji wa klabu
hiyo, Hajji Manara amewataka wapenzi na mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi
kuishangili timu yao ili kuwapa nguvu na hamasa wachezaji kuibuka na ushindi.
No comments