BUKU 5 TU KUWAONA YANGA NA ST LOUIS
Yanga sc imetaja
viingilio vitatu katika mchezo wake wa hatua ya awali wa klabu bingwa barani
Afrika dhidi ya Saint Louis FC ya Shelisheli siku ya Jumamosi katika Uwanja wa
Taifa Dar es salaam.
Kiingilio cha chini katika
mchezo huo kwa majukwaa ya mzunguko itakuwa 5000 wakati VIP B na C Itakuwa Sh
7000 huku VIP A ikiwa Sh 10000
Waamuzi wa mchezo huo wanatarajiwa kutoka
Ethiopia na Kamishna wa mchezo akitokea nchini Namibia, Mwamuzi wa kati atakuwa
Belay Tadesse Asserese akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Tigle Gizaw
Belachew na mwamuzi msaidizi namba mbili Kinfe Yilma Kinfe wakati mwamuzi wa
akiba atakuwa Amanuel Heleselass Worku na Kamishna Frans Vatileni Mbidi.
No comments