MECHI TATU KUPIGWA LEO LIGI KUU ENGLAND, ARSENAL NA LIVERPOOL VIWANJA TOFAUTI.

Alex Iwobi and new signing Henrikh Mkhitaryan compete for the ball during Arsenal training
Ligi kuu ya Soka Nchini England inaendelea leo usiku kwa mechi 3 kuchezwa kwenye viwanja vitatu nchini humo huku Arsenal na Liverpool zote zikisaka pointi 3 muhimu.

Liverpool baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Swansea itakua ugenini kujitafakari ikiwa pia kupunguza machungu ya kutupwa nje ya michuano ya kombe la FA itakapocheza na wenyeji Huddesfield Town 

Swansea ambao walifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Liverpool katika mechi iliyopita watakuwa tena nyumbani kuwakabili vinaja wa Arsene Wenger ambao wamekua moto kweli tangu kuondoka kwa mshambuliaji wao Alexis Sanchez huku Arsenal wakitarajiwa kumuanzisha kwa mara ya kwanza Henrik Mkhtaryan aliyehamia klabu hiyo akitokea Manchester United.

Jijini London leo kutachezwa mchezo wa dabi ya London baina ya West Ham na Crystal Palace mechi inayoonekana itakua na upinzani mkubwa kutokana na matokeo mazuri ya timu hizo baada ya kujinusua kushuka daraja

MECHI ZOTE HIZO ZITAANZA SAA 5 KASOROBO ISIPOKUA MECHI YA LIVERPOOL ITAKAYOANZA SAA 5 KAMILI USIKU KWA SAA ZA HAPA NYUMBANI 

No comments

Powered by Blogger.