JULIO ATAMBA KUITUPA NJE MWADUI FA LEO

Kocha mkuu wa timu ya Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo 'Julio' ametamba kuitoa kwenye mashindano timu yake ya zamani ya Mwadui FC katika michuano ya Azam Sports Federation Cup watakapo kutana jioni ya leo.

Dodoma ya Julio itashuka katika uwanja wa Mwadui Complex katika mchezo wa FA hatua ya 16 bora unaosubiriwa kwa hamu na wadau wa soka mkoani Shinyanga.

Julio amesema anawafahamu vizuri Mwadui jinsi wanavyocheza na atatumia mapungufu yao kuwaua katika uwanja wao wa nyumbani.

"Ni matumaini yangu leo tutashinda, tumejipanga kwa hilo wachezaji wapo kwenye hali nzuri tunasubiri muda ufike tuingie uwanjani," alisema kocha huyo mwenye maneno mengi.

Julio aliacha kuifundisha Mwadui miezi kadhaa iliyopita baada ya kukiri waamuzi hawachezeshi kwa haki kabla ya kutimkia Dodoma FC.

No comments

Powered by Blogger.