KAA MBALI NA ZANZIBAR, YAIVUA UBINGWA UGANDA NA KUTINGA FAINALI CHALLENJI
Timu ya
Taifa ya Zanzibar imeendelea kuonyesha ubabae wake kwa kuivua Ubingwa mabingwa
watetezi wa michuano ya kombe la Challenji Uganda kwa kuifunga kwa bao 2-1
katika pambano la pili la Nusu fainali ya michuano hiyo inayoendelea Nchini
Kenya.
Abdulazizz Makame alitangulia kuipatia Zanzibar bao la kwanza dakika ya 22 ya mchezo lakini mfungaji bora wa michuano hiyo mpaka sasa Derrick Nsibambi wa Uganda aliisawazishia timu yake bao hilo dakika ya 38 na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko timu zote zikiwa suluhu ya bao 1-1.
Kipindi cha pili Zanzibar waliongeza nguvu ya mashambulizi na harakati zao zikazaa penati ambayo ilifungwa kiufundi na Kiungo Mohammed Banka dakika ya 57 bao ambalo liliipa Zanzibar tiketi ya kucheza fainali ya michuano hiyo mikubwa katika ngazi ya nchi za Afrika mashariki na Kati mchezo huo baina ya Zanzibar na Uganda ulipigwa katika dimba la MOI Kasarani.
Zanzibar ambayo wengi hawakuitegemea inaingia fainali ambapo itakutana na wenyeji Kenya ambao wametinga fainali baada ya kuifunga Burundi bao 1-0 na fainali itachezwa Jumapili hii ya tarehe 17 Disemba 2017 katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakoss
Zanzibar na Kenya zote zilikua katika kundi A na katika mechi yao ya kundi hilo ilimalizika kwa sare ya bila kufungana hivyo mpambano wa Jumapili unatarajiwa kuwa ni wa kuvutia mno.
No comments