MOHAMMED SALAH NDIYE MCHEZAJI BORA EPL NOVEMBA
Winga machachari wa kimataifa wa Misri anayeichezea Liverpool Mohammed Salah amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba katika tuzo za kila mwezi zinazotolewa katika ligi kuu ya England.
Salah mchezaji wa zamani wa Chelsea ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwa na mwezi mzuri zaidi akifunga bao 7 katika mechi 4 za timu yake katika mwezi huo
Mpaka sasa Mohammed Salah ameshafunga mabao 20 kwa timu yake tangu ajiunge nayo kwa ada ya uhamisho paundi milion 30 akitokea AS Roma
No comments