SPURS HALI SI NZURI YADUNDWA NA LEICESTER, NEWCASTLE YAWACHOMOLEA WEST BROM
Mzunguko wa 14 wa ligi kuu ya England ulianza jana kwa mechi nne kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini England ambapo Tottenham walikumbana na kichapo ugenini huku Newcatsle wakizinduka na kuambulia sare.
Tottenham ikicheza katika uwanja mgumu wa King Power nyumbani kwa Leicester City Tottenham walikubali kichapo cha bao 2-1 toka kwa wenyeji ambao jana walionekana wakiwa katika ubora wao mabao ya City yakifungwa na Jermie Vardy na Riyad Mahrez huku Harry Kane akifunga bao la kufutia machozi la Tottenham.
Newcastle United wakicheza nyumbani baada ya vipigo mfululizo katika ligi hiyo jana walishangazwa na bao 2-0 ambazo West Brom walitangulia kuzipata kupitia kwa Hal Robson Kanu na Sam Field lakini kikosi cha kocha Raphael benitez kilizinduka na kurejesha magoli yote mawili yakifungwa na Ciaran Clack na goli la kujifunga la nahodha John Evans.
Brighton wakiwa nyumbani walishindwa kufurukuta na kulazimishwa sare na timu inayoshika mkia Crystal Palace kwa kutoka sare ya bila kufungana mchezo uliokua wa vuta ni kuvute.
Manchester United ikisafiri ugenini iliweza kuibuka na ushindi wa bao 4-2 dhidi ya Watford taarifa kamili ya mchezo huo unaweza kuipata kwa kubofya hapa http://www.wapendasoka.com/2017/11/ashley-young-apiga-bao-2-man-united.html
No comments