IMEVUJA: EVERTON KUMTANGAZA BIG SAM KAMA KOCHA MPYA

Sam Allardyce will be announced as the new Everton manager in the next 48 hours
Habari ambazo hazijathibitishwa na klabu ya Everton ni uteuzi wa kocha mpya wa klabu hiyo ambaye anatajwa kuwa ni mkufunzi wa zamani wa England Sam Allardyce ambaye yuko katika mazungumzo ya mwisho na huenda leo au kesho akatangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.

Sam Allardyce maarufu kama Big Sam amekua nje ya ulingo wa soka tangu alipotimuliwa kuinoa timu ya taifa ya England kwa kashfa na sasa atarejea kutaka kurudisha heshima yake pia kuiepusha Everton na balaa la kushuka daraja.

Tangu walipomtimua kocha Ronald Koeman mwezi Uliopita Everton wamekua wakihaha kutafuta mbadala wake huku nguvu kubwa ilikua imewekwa kwa kocha wa Watford Mreno Marco Silva na baada ya kushindwana nae wameona wamkabidhi sasa timu mzawa ambaye ili kurejesha heshima klabuni hapo.

 

No comments

Powered by Blogger.