SHIZA KICHUYA AIREJESHA SIMBA KILELENI VPL
Wekundu wa Msimbazi Simba wamerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City katika pambano lililopigwa katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.
Shiza Ramadhani Kichuya ndiye aliyefunga bao pekee la Simba katika mchezo wa Leo bao alilofunga dakika ya 7 ya mchezo akipokea pasi ya Jonas Mkude ambaye Leo alianza katika nafasi ya kiungo akichukua nafasi ya James Kotei ambaye leo alicheza kama beki.
Bao la Kichuya limelalamikiwa na Mbeya City wakidai mfungaji alikua ameotea.
Matokeo ya Leo yanaifanya Simba kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara wakifikisha pointi 19

No comments