ARSENAL NAYO YAKUMBANA NA KIPIGO KWA MAN CITY

City's new record scorer Sergio Aguero added another to his tally when he converted a second half penalty
Manchester City Imeendelea kugawa dozi kwa timu zote inazokutana nazo msimu huu baada ya kuifunga Arsenal kwa bao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Soka nchini England uliopigwa katika dimba la Etihad jijini Manchester.

Kevin De Bryune alitangulia kuipatia Manchester City bao la kwanza dakika ya 19 ya mchezo bao lililodumu mpaka mapumziko kisha Sergio aguero akafunga bao la pili dakika ya 50 kabla ya Gabriel Jesus hajaifungia City bao la tatu na arsenal walipata bao la kufutia machozi dakika ya 65 likifungwa na Alexandre lacazette.

No comments

Powered by Blogger.