HAWA HAPA WANAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AFRICA KWA MWAKA 2017
Shirikisho
la soka barani Afrika limetoa orodha ya wachezaji 30 watakaowania taji la
mchezaji bora wa soka barani Afrika kwa mwaka 2017.
Mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya
Tanzania Mbwana Samatta anaechezea Krc Genk ya Nchini Ubeligiji nae
ameorodheshwa kwa mara ya pili
Mshindi wa mwaka 2016 Riyad Mahrez wa Algeria
hakuorodheshwa katika orodha hiyo.
Kati ya wachezaji 30 waliorodheshwa ni saba
pekee ambao hawachezi soka yao barani Ulaya, huku kipa wa Misri Essam EL Hadary
akiorodheshwa.
Washindi wa mataji hayo watatangazwa katika
mji mkuu wa Ghana Accra mnamo tarehe 4 mwezi January 2018.
Kura zitakazopigwa na makocha, wakurugenzi wa
kiufundi kutoka mataafa mbali mbali pamoja na wanachama wa kiufundi wa Caf na
kamati endelebu mbali na jopo la waandishi zitabaini washindi.
Vincent Aboubakar
(Cameroon & Porto), Karim El Ahmadi (Morocco na Feyenoord), Christian Atsu
(Ghana & Newcastle), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon na Borussia
Dortmund), Eric Bailly (Cote d'Ivoire na Manchester United), Cedric Bakambu (DR
Congo na Villareal), Keita Balde (Senegal & Monaco), Christian Bassogog
(Cameroon na Henan Jianye), Yves Bissouma (Mali na Lille), Khalid Boutaib
(Morocco na Yeni Malatyaspor), Yacine Brahimi (Algeria na Porto), Essam El
Hadary (Egypt na Al Taawoun), Junior Kabananga (DR Congo na Astana), Fackson
Kapumbu (Zambia na Zesco), Naby Keita (Guinea na RB Leipzig), Ali Maaloul (Tunisia
na Al Ahly), Sadio Mane (Senegal na Liverpool), Moussa Marega (Mali na Porto),
Victor Moses (Nigeria na Chelsea), Youssef Msakni (Tunisia na Al Duhail),
Michael Olunga (Kenya na Girona), Fabrice Ondoa (Cameroon na Sevilla), Denis
Onyango (Uganda na Mamelodi Sundowns), Thomas Partey (Ghana na Atletico
Madrid), Mohamed Salah (Egypt na Liverpool), Mbwana Samata (Tanzania na Genk),
Jean Michel Seri (Cote d'Ivoire na Nice), Percy Tau (South Africa na Mamelodi
Sundowns), Bertrand Traore (Burkina Faso na Lyon), William Troost-Ekong
(Nigeria na Bursaspor)
No comments