SPURS YAICHARAZA REAL MADRID NA KUTINGA 16 BORA

Tottenham Hotspur imewashushia kipigo mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa Ulaya Real Madrid cha mabao 3-1
Spurs wamefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora baada ya ushindi huo katika uwanja wa Wembley.

Dele Alli alifunga magoli mawili na Ericksen huku goli pekee la mabingwa hao likifungwa na Cristiano Ronaldo, Real wamefungwa kwa mara ya kwanza kwenye hatua za makundi toka mwaka 2012 na kipigo cha pili ndani ya wiki moja baada ya kupoteza mchezo wa ligi dhidi ya Ginora
Matokeo yote ya klabu bingwa barani ulaya jana

Borussia Dortmund 1-1 APOEL

Liverpool 3-0 Maribor

Sevilla 2-1 Spartak Moscow
Besiktas 1-1 Monaco

FC Porto 3-1 RasenBallsport Leipzig

SSC Napoli 2-4 Manchester City

Shakhtar Donetsk 3-1 Feyenoord


No comments

Powered by Blogger.