ERASTO AWAFUNIKA OKWI, NIYONZIMA SIMBA, MWEZI OKTOBA
Mchezaji
kiraka wa timu ya Simba Erasto Nyoni atapokea kitita cha sh laki tano (500,000)
baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa mabingwa hao wa
kombe la FA.
Erasto
ambaye mara kadhaa kocha Joseph Omog amekuwa akimtumia kama beki wa kulia au
kushoto yupo kwenye kiwango bora msimu huu ambapo mchango wake ni mkubwa
kikosini.
Licha ya
uwepo wa nyota wenye majina makubwa kama Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima, John Bocco
na Shiza Kichuya lakini jina la Nyoni huwezi kukosa kulisikia kila baada ya
kumalizika kwa mchezo wa Wekundu hao.
Erasto ni
mmoja wa wachezaji wa Simba wanaotarajiwa kuwepo kwenye kikosi kitachocheza na
Mbeya City mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya mwishoni
mwa juma.
Nyoni ndiye
mchezaji aliyedumu muda mrefu kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania
'Taifa Stars' ambapo huu ni mwaka wa 10 bado anaendelea kujumuishwa.
No comments