BARCELONA YABANIWA KUFUZU UGENINI, JUVENTUS NAYO YAAMBULIA SARE MABINGWA ULAYA

Argentine ace Messi vies for possession of the ball in central midfield alongside Olympiacos's Kostas Fortounis
Mechi mbili za Kundi D katika ligi ya mabingwa Ulaya zilimalizika kwa sare na timu nne kugawana pointi moja moja ambapo sasa watasubiri mpaka mechi zijazo kuamua timu zipi zitafuzu kwa hatua inayofata ya 16 bora kwenye ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Barcelona ambayo wengi walitegemea ingefuzu jana ililazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji Olympiacos katika mechia mabayo wenyeji walimtegemea sana kipa wao kuweza kuwapa pointi hiyo moja muhimu huku kasi ya washambuliaji wa Barcelona waliokua wakiongozwa na Lionel Messi na Luis Suarez.

Juventus ambao ni mabingwa wa Italia wao walisafiri mpaka Ureno kuwavaa Sporting Lisbon na hali haikua rahis kwao kwani walitakiwa kusawazisha bao la mapema lililofungwa na Bruno Cesar kupata sare ya bao 1-1 huku Gonzalo Higuain akiwa ndiye mwokozi wa Juventus.

Matokeo ya jana yanalifanya kundi D kuendelea kuwa gumu kwani Barcelona wenye pointi 10 bado hawana uhakika wa kufuzu kwani Juventus wanawafatia wakiwa na pointi 7 huku Sporting Lisbon wakiwa na pointi 4 na Olympiacos wanashika mkia na pointi yao moja waliyoipata kwa Barcelona zikiwa zimebaki mechi mbili kwa kila timu.

No comments

Powered by Blogger.