MAN UNITED YAJIWEKA PAZURI KUFUZU 16 BORA, FC BASEL YABANIWA NYUMBANI MABINGWA ULAYA

Douglas offered a constant threat with his dribbling ability and United struggled to contain the technically-gifted player 
Mabingwa wa kombe la Europa Manchester united wameendelea kupata ushindi 100% katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu hatua ya makundi baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Benfica toka Ureno mchezo wa kundi A wa michuano hiyo uliopigwa katika dimba la Old Trafford.

Goli la kujifunga la kipa wa Benfica Mile Svilar liliwapa man United uongozi katika mechi hiyo na kumaliza kipindi cha kwanza United ikiwa mbele kwa bao 1-0 huku ikishuhudiwa Antony Martial akikosa penati.

kipindi cha pili United iliwatoa Juan Mata,Jesse Lingard na Antony Martial na nafasi zao kuchukuliwa na Ander Herrera,Henrik Mkhtaryan na Marcus rashford mabadiliko yaliyoongeza kasi na upatikanaji wa bao la pili lililofungwa na Daley Blind kwa penati baada ya Marcus Rashford kuangushwa kwenye eneo la hatari.

Mechi nyingine katika kundi hilo FC Basel ikiwa nyumbani ilinyukwa bao 2-1 na wageni CSKA Moscow toka Russia na kuzifanya timu hizo mbili zote kufikisha pointi 6 na kuichelewesha kwa muda Manchester United kufuzu kwa hatua ya 16 bora kwani yenyewe ina pointi 12 mpaka sasa inahitaji sare tu and hizo timu mbili moja ifungwe ili ifuzu

No comments

Powered by Blogger.