PSG YAPIGA 5 YAFUZU, BAYERN MUNICH NAO WAFUZU 16 BORA MABINGWA ULAYA

Verratti celebrates scoring his first Champions League goal since September 2014 with Neymar and Mbappe
Moja kati ya makundi yaliyoonekana kuwa magumu ni kundi B katika ligi ya mabingwa Ulaya ambapo Uwepo wa PSG, Celtic, Bayern Munich na Anderletch ilionekana kuwa isingekuwa rahisi kwa timu kufuzu lakini mpaka sasa zikiwa zimebaki mechi mbili kwa kila timu tayari PSG na Bayen Munich zimeshafuzu kwa hatua ya 16 bora baada ya kuibuka na ushindi katika mechi zao jana Usiku.

PSG waliibuka na ushindi wa bao 5-0 wakiwa nyumbani dhidi ya mabingwa wa Ubelgiji Anderletch magoli matatu ya beki wa kushoto Layvin Kurzawa huku Neymar na marco Veratti wakifunga bao moja kila mmoja kufanikisha ubingwa wa nne mfululizo msimu huu katika ligi ya mabingwa huku wakiweka pia rekodi ya kufunga mabao mengi bila kufungwa bao lolote mpaka sasa wakiwa wameshafunga mabao 17.

Bayern Munich ikisafiri mpaka Scotland iliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya wenyeji Celtic matokaeo yanayoifanya bayern Munich kufikisha pointi 9 ikishika nafasi ya pili nyuma ya PSG wanaoongoza wakiwa na pointi 12 huku Celtic wakibaki na pointi 3 katika nafasi ya 3 huku Anderletch wakikamata mkia.

No comments

Powered by Blogger.