SPORTPESA YAZINDUA PROMOSHENI YA SHINDA NA SPORTPESA
| Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Bwana Tarimba Abbas |
Kampuni ya michezo ya kubashiri nchini ya SportPesa
jana Oktoba 25 imezindua rasmi kampeni ya SHINDA NA SPORTPESA itakayodumu kwa
siku 100 ambapo mshindi mmoja ataweza kujishindia TVS KING mpya kila
siku.
Kwenye promosheni hiyo, sambamba na washindi
kuondoka na TVS KING mpya kila siku, lakini pia kutakuwa na zawadi nyingine
zinazoshindaniwa ambazo ni pamoja na tiketi tatu kwenda nchini Uingereza
kutazama mechi ya EPL, tiketi moja ikitolewa kilamwezi sambamba na jezi orijino zitakazotolewa kila
wiki.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa promosheni hiyo
uliofanyika kwenye Uwanja wa Bakhresa, Manzese jijini Dar es Salaam asubuhi ya
leo, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Bwana Tarimba Abbas
amesema kuwa promosheni hiyo ina lengo la kubadili maisha ya watanzania
kiuchumi.
“Sisi kama kampuni tumeona umuhimu wa kuja na
promosheni hii ili kuweza kuwainua wateja wetu kiuchumi na kuwaongezea fursa ya
kujipatia kipato zaidi. Kama ulikuwa na TVS KING moja basi tunakuongezea ya
pili ili uongeze kipato zaidi na kama ulikuwa huna kabisa basi tunakupa hii
moja ili uanze leo.
Jinsi ya kushiriki
Baada ya kusema hayo, Bwana Tarimba alitoa ufafanuzi
jinsi ya kushiriki kwenye promosheni hiyo ili kuweza kushinda TVS KING mpya
kama ifuatavyo; “Kwanza ni lazima tukumbuke kuwa kila siku kutakuwa na
mshindi hivyo watakaopata fursa ya kushinda ni wale watakaokuwa wakicheza na
SportPesa tu. “Kama bado hujawahi kucheza na SportPesa basi hakikisha
unajisajili kwa kutuma neno GAME kwenda 15888 na baada ya hapo utatakiwa kuweka
pesa kwenye akaunti yako ya SportPesa kwa namba ya biashara 150888 kisha piga
*150*87# au tembelea www.sportpesa.co.tz KUWEKA UTABIRI wako mara nyingi zaidi
ili uweze kuingia kwenye droo.
“Hakuna uchawi mwingine wa kushinda TVS KING mpya
zaidi ya kuweka ubashiri wako na SportPesa na hii ni fursa pekee ya kujiajiri
na kubadili maisha yako kwasababu sote tumekuwa mashahidi jinsi ambavyo vijana
wengi leo hii wamejiajiri au kuajiriwa kupitia TVS KING.
Hii itakuwa ni promosheni ya pili kutangazwa na
Kampuni ya SportPesa ambayo ni mdhamini mkuu wa klabu za Simba, Yanga na
Singida United baada ya ile ya kwanza ya Zali la Mwanaspoti itakayodumu kwa
wiki nane ambayo kila wiki mshindi mmoja
anajishindia tiketi ya kwenda nchini Uingereza
kutazama mechi ya EPL huku mshindiwa kwanza akiwa ameshapatikana.
No comments