KOCHA WA ZAMANI SOUTHAMPTON ATEULIWA KUINOA LEICESTER CITY.

Klabu ya Leicester City imemteua kocha wa zamani wa Southampton Claude Puel kama kocha wao mpya Kwa mkataba wa miaka mitatu kuwanoa Mabingwa hao wa mwaka 2016 Katika ligi kuu ya England.

Puel anaziba nafasi iliyoachwa wazi na  kocha Craig Shakespeare ambaye alitimuliwa wiki iliyopita baada ya matokeo mabaya kwenye michezo yake ya hivi karibuni kwenye ligi kuu ya England ambaye anakua kocha wa tatu kuifundisha Leicester City mwaka huu.

Puel raia wa Ufaransa mwenye miaka 56 aliiwezesha Southampton kumaliza katika nafasi ya 8 msimu uliopita sambamba na kuifikisha katika fainali ya kombe la Ligi ambapo walifungwa na Manchester United

No comments

Powered by Blogger.