CARABAO CUP : CHELSEA YATINGA ROBO FAINALI, SPURS YATUPWA NJE.

Mechi mbili za mwisho kuwania nafasi ya kucheza robo fainali ya michuano ya kombe la ligi nchini England maarufu kama CARABAO CUP zilichezwa Jana usiku nchini humo. 

Chelsea wakiwa nyumbani Darajani waliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Everton mabao ya beki wa kimataifa wa Ujerumani Antony Rudieger na kiungo wa Brazil Willian huku Everton ambao Juzi walimtimua kocha wao Wakipata bao la kufutia machozi kupitia Kwa mshambuliaji Calvert-Lewin. 
Katika mechi nyingine hiyo Jana Tottenham Hotspur wakiwa nyumbani Wembley walikubali kichapo cha bao 3-2 toka kwa West Ham na kushangaza wengi kwani Tottenham Hotspur walikua wakiongoza Kwa bao 2-0 mpaka mapumziko. 

Kazi nzuri iliyofanywa na Andre Ayew mtoto wa Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ghana Abeid Pelle ndiyo iliyowapa West Ham ushindi huo kwani Ayew alifunga mabao mawili dakika za 55 na 60 akisawazisha mabao ya Spurs yaliyofungwa na Moussa Sissoko na Delle Alli huku Obinze Ogbonna akifunga bao la ushindi dakika ya 70

Kwa matokeo hayo West Ham na Chelsea wanaungana na Manchester United ambao ni Mabingwa watetezi,  Manchester City, Bristol City, AFC Bournemouth, Leicester City na Arsenal katika hatua ya robo fainali ambayo ratiba yake itapangwa Leo Alhamis na kurushwa moja Kwa moja kupitia vituo mbalimbali vya luninga lakini pia kupitia ukurasa maalumu wa Carabao mtandao wa Twitter ambao ndiyo wadhamini wakuu wapenda soka wanaweza kuona moja kwa moja katika

No comments

Powered by Blogger.