REAL MADRID YAMTENGEA PAUNDI MILIONI 177 HARRY KANE WA SPURS
Habari toka nchini Spain zimeeleza kwamba Mabingwa wa La Liga Real madrid wanajiandaa kupeleka dau la paundi milioni 177 sawa na Euro milioni 200 kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa England anayeichezea Tottenham Hotspur Harry Kane.
Harry Kane mshindi wa tuzo ya mfungaji bora wa lighi kuu ya England kwa misimu miwili mfululizo anatajwa kama mshambuliaji wa kwenda kumaliza tatizo la Ushambuliaji kwenye klabu ya Real Madrid na hii inatokana na uongozi wa mabingwa hao wa Ulaya kutoridhishwa na kiwango cha Mshambuliaji aliyepo kikosini hivi sasa Karim Benzema.
Mipango ya Usajili huo itafanyika katika majira yajayo ya kiangazi lakini bado haijafahamika Kama Tottenham Hotspur watakubali kumwachia nyota wao huyo ikizingatiwa wakati huo watakua wakihamia kwenye uwanja wao wa White Hart Lane baada ya ukarabati.
No comments