MESSI AONGOZA MAZOEZI YA ARGENTINA TAYARI KUSAKA NAFASI YA KUCHEZA KOMBE LA DUNIA
Mshambuliaji wa Argentina na nahodha wa nchi hiyo Lionel Messi ameonekana akiwa na furaha wakati wa mazoezi ya timu yake hiyo ya taifa tayari kawaajili ya pambano lao muhimu la kuwania kufuzu kwa kombe la dunia mwakani nchini Russia.
Argentina itacheza dhidi ya Peru Ijumaa wiki hii katika mchezo ambao ushindi atakua ni nafasi nzuri kwa argentina kutinga moja kwa moja katika fainali zijazo za kombe la Dunia na kama watafungwa basi itawabidi kujaribu bahati yao ya kufuzu kwa njia ya mtoano.
Peru inakamata nafasi ya 4 huku Argentina ikikamata nafasi ya 5 katika msimamo wa timu zinazowania nafasi tano za kufuzu kwa kombe la Dunia mwakani bara la Amerika kusini.
Baada ya mechi hiyo Argentina itacheza dhidi ya Ecuador kukamilisha mechi zake na kama itasalia katika nafasi hiyo ya 5 basi itabidi kucheza mechi ya mtoano dhidi ya New Zealand.
Sergio Kun Aguero ataikosa mechi hiyo kwani atakua nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita kufuatia ajali ya gari nchini Uholanzi
No comments