MESSI APIGA 2 BARCELONA IKIIBUKA NA USHINDI NOU CAMP BILA MASHABIKI
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ameibuka shujaa katika ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Las Palmas katika mchezo wa ligi kuu ya Spain La Liga.
Mchezo almanusura uahirishwe kutokana na sababu za kiusalama kwenye jimbo la Catalunya leo na hii inatokana na vurugu kubwa zilizozuka kati ya polisi na waandamanaji wanaotaka kujitenga na serikali ya Spain.
Licha ya mchezo huo kuruhusiwa kucheza lakini mashabiki walizuiwa kuingia katika uwanja wa Nou Camp mmoja kati ya viwanja vinavyoingiza idadi kubwa ya mashabiki.
Sergio Busquet alitangulia kuipatia Barcelona bao la kwanza dakika ya 49 kabla ya Lionel Messi hajafunga dakika ya 70 na 77 kukamilisha ushindi huo ambao unazidi kuwaweka Barcelona Kileleni mwa msimamo wakifikisha pointi 21 wakiwa wameshinda mechi zote 7 walizocheza.
No comments