NEWCASTLE NA LIVERPOOL HAKUNA MBABE


Mechi baina ya Liverpool waliokua ugenini dhidi ya Newcastle imemalizika kwa sare ya bao 1-1 katika uwanja wa St. James Park.

Philipe Coutinho alitangulia kuipa goli Liverpool kwa shuti kali umbali wa mita zaidi ya 20 dakika ya 29 ya mchezo kabla ya Joselu hajaisawazishia Newcastle United bao dakika ya 36.

Matokeo hayo yanaifanya Newcastle kufikisha pointi 10 katika nafasi ya 9 huku Liverpool wakifikisha pointi 12 katika nafasi ya 7.

Matokeo mengine leo Arsenal wameibuk na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Brighton wakati Everton wamefungwa nyumbani 1-0 na Burnley.

No comments

Powered by Blogger.