MAN UNITED YAIADABISHA SPURS MAPEMA TU


Mechi ya mapema kabisa katika ligi kuu Soka ya England baina ya Wenyeji Manchester United dhidi ya Tottenham Hotspur imemalizika Kwa United kushinda bao 1-0.

Mchezo huo umemalizika muda mchache uliopita kwenye dimba la Old Trafford kushuhudia Man United ikipata bao pekee dakika ya 81 na Anthony Martial ambaye alikua na dakika chache uwanjani akiingia kuchukua nafasi ya Marcus Rashford.

Licha ya kufungwa Tottenham ilionekana kuwa bora muda wote japokua walimkosa nyoka wao Harry Kane ambaye ni majeruhi.

Matokeo haya yanaifanya United kufikisha pointi 23 Ikiwa ni pointi 2 nyuma ya vinara Manchester City wanaocheza badae dhidi ya West Bromwich huku Spurs wakibaki na pointi zao 20.

No comments

Powered by Blogger.