KIJIWE CHA WAPENDA SOKA : FIKRA ZA WAPENDA SOKA KATIKA PAMBANO LA UNITED VS SPURS NA YANGA VS SIMBA

Image result for man united vs tottenham
Karibu tena mdau katika kona yetu ya Kijiwe cha Wapenda soka ambapo leo Wapenda Soka kupitia group la Whatsapp waliweza  kujadili mengi yahusuyo michezo miwili ya Leo Katika  Soka hapa Bongo na nchini England.

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Yanga wataikaribisha Simba katika uwanja wa Uhuru wakati nchini England ni Manchester United vs tottenham

Haya ni machache Kati ya yaliyojadiliwa KIJIWENI Leo

.... Ameandika Sylva

Simba vs Yanga
Tofauti na watu wengi hasa mashabiki wanavyoitazamia. Tunaweza shuhudia mpira uliopooza kupita mechi zote msimu huu. Hii ni kwa sababu tu timu hizi kuwa na viwango vinavyofanana na hasa ukiangalia kasi zao kwenye mechi zao za kawaida zilizopita. Watu wa kuwaangalia kwa upande wa Simba ni Okwi, Mzamiru na Erasto Nyoni. Kwa upande wa Yanga kuna Ajib, Tambwe na Tshishimbi..
Simba wanatakiwa kutomuanzisha John Bocco kwenye mashambulizi kama wanataka ushindi.

Natabiri  Matokeo kuwa  ni Simba 0 Yanga 0

MAN UNITED VS TOTTENHAM
 Licha ya utd kuwa mbabe kwa miaka mingi wakikutana na spurs, kwa sasa hali ni tofauti sana kwani hawana tena ile kasi ya kipindi cha nyuma. Hakuna timu inahofia kucheza na utd kwa sasa ndio maana hata Bristol city wameshangilia sana kupangwa nao kwenye carabao cup.

 Spurs wanashambulia kwa kasi sana kwa kuwa pia wana washambuliaji wenye kasi. Lakini mechi ya leo itaamuliwa na magolikipa mahiri wa timu zote mbili. Hugo lloris na David de gea.

 Matokeo ni Utd 0 Spurs 0

... Ameandika Fes Arsenal

Man utd vs Tottenham
Kama kweli man utd anahitaji kuwa kwenye mbio za wanaogombania ubingwa kwa uhakika anapaswa kupata matokeo ya ushindi tu dhidi ya timu ngumu Spurs leo.

Naiona kama mechi ngumu sana kwa Man utd kwa sababu ya ubora walionao Totenham. Man utd atakuwa na faida ya uwanja wake wa nyumbani anapaswa kuutumia vema ili apate matokeo

Utabiri wangu Man utd 1:1Totenham

YANGA VS SIMBA

 Kihisia hata hauelezeki huu mpambano Ila unapaswa uwe mchezo mzuri kwa sababu una hamasa kubwa kama vile Ajib vs Okwi Kufungana kwa points Wote wapo kileleni Mwamuzi bora wa msimu uliopita ndiye amepewa kipyenga leo naamini atachezesha kwa umakini mkubwa sana.

Yanga watapaswa kuwa makini sana maana kuna baadhi ya wachezaji wao muhimu hawatakuwepo kama vile Kamusoko. Simba wanayopresha kubwa sana ndani na nje ya uwanja hadi benchi la ufundi kwa sababu ya thamani ya kikosi chao Yanga wakitumia fursa hii watamfunga Simba

 Utabiri wangu Yanga 1:2 Simba

...Ameandika Ahmed Zein

MANUTD vs SPURS

 Uzuri wa Epl kila wiki kuna BIG mechi na hii ndio raha yake. Twende katika uchambuzi wa Big mechi ya leo. ManUtd Leo wapo uwanjani kwao OT, mimi timu ikiwa nyumbani huwa nasema iko uwanja wa maringo kwa hiyo United wana nafasi kubwa ya kushinda kwa kuwa wapo nyumbani. Nikiangalia record ya nyuma ya United kufungwa na HUD hapa naweza sema United walifungwa kizembe, leo hawatakiwi kurudia makosa hasa ukiangalia spurs wanawachezaji wakali wenye kutumia nafasi ndogo inayopatikana.

Vile vile Mo ni moja wa makocha wanaopenda mind game hope leo hataki kupoteza kabisa. SPURS Wamekuwa na record nzuri sana ya kushinda mechi za ugenini tangu msimu umeanza. Kwa kiwango walichokionyesha kule Uefa dhidi ya Madrid na pia kuifunga liverpool ni wazi kabisa spurs kwa sasa wameimarika.

 Kumkosa Harry Kane kutapunguza makali yao lakini kutampa nafasi Lorrente kuonyesha cheche zake leo. Tukiangalia msimamo wa ligi timu zote mbili zimefungana point 20.

Utabiri wangu ManUtd 1-2 Spurs

Ameandika Edo D.C.

Moja Kati ya siku nzuri sana Leo Kwa sisi Wapenda Soka kwani ni siku ambayo imewatawliwa na hisia kila kona kuona timu ipi itaibuka na ushindi.

Kufungana Kwa pointi Kwa timu zote zinazopambana Leo kunaleta ladha nzuri ya kushuhudia nani ataweza kukenua meno baada ya dakika 90.

MAN UNITED Iko Old Trafford uwanja ambao United haijapoteza mchezo msimu huu na iaingependa kupoteza kirahisi na hasa ikichangiwa na matokeo ya kufungwa bao 2-1 katika mchezo uliopita dhidi ya Huddersfield mechi ambayo makosa mawili ya Juan Mata na Victor Linderlof yaliwapa Huddersfiel zawadi ambayo vizazi vilikua Vikisubiri kushuhudia.

Kukosekana Kwa Harry Kane sio shida Kwa Spurs hasa ikizingatiwa kwamba Mousa Dembele amerejea katika nafasi ya kiungo mchezaji ninayemwona kuwa ni msumbufu Mno awapo uwanjani ni kama Pogba kwenye kikosi cha United.

Kurudi Kwa Eric Bailly kunamfanya kurejea katika nafasi ya ulinzi na ni mechi ambayo Mourinho hatakubali kupoteza  kirahisi na tunaweza kushuhudia akishambulia dakika zote.

Hapa Bongo Mara nyingi mechi hizi za watani wa jadi hutawaliwa na mambo mengi zaidi ya ufundi uwanjani ila naiona Simba ambayo inaingia ikiwa na nguvu kubwa ya kuibuka na ushindi.

Kikosi chao kinachoanza Leo kina wachezaji watano raia wa kigeni Hawa ndiyo wanaweza kuimaliza Yanga mapema. Okwi, Mavugo na Niyonzima ni wachezaji wa daraja la juu na uzuri washacheza sana mechi hizi hivyo inawapa nafasi kubwa ya kuthibitisha ubora wao.

NATABIRI TIMU ZINAZOTUMIA RANGI NYEKUNDU KUSHINDA 3-1 LEO.

No comments

Powered by Blogger.