YANGA NA SIMBA HAKUNA MBABE, KICHUYA AENDELEA KUITESA YANGA
Shiza Ramadhani Kichuya ameendelea Kuitesa Yanga akifunga bao la Simba katika sare ya bao 1-1 katika mchezo wa watani wa Jadi wa Soka la Tanzania Yanga waliokua Wenyeji dhidi ya Simba.
Mchezo huo wa ligi kuu Soka Tanzania bara ulichezwa kwenye dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo mpaka mapumziko hakuna aliyeweza kuzifumania nyavu za mwenzake.
Shiza Kichuya alifungua Akaunti ya mabao Simba akifunga bao la kwanza dakika ya 57 baada ya kazi nzuri ya Emmanuel Okwi aliyeupiga mpira hafifu na kipa wa Yanga kushindwa kuokoa mpira na kumtengenezea Erasto Nyoni ambaye alimwekea Shiza Kichuya na kufunga bao Hilo.
Hii si Mara ya kwanza Shiza Kichuya amekua kuwafunga Yanga baada ya kufanya hivyo kila walipokutana.
Ushindi wa Simba haukuchukua hata dakika kwani Yanga walifanya shambulizi la Nguvu na kufanikisha kupata bao la kusawazisha baada ya uzembe wa kipa wa Simba na beki wake Juuko Murshid kushindwa kuokoa mpira wa Geofrey Mwashiuya na bila ajizi Obrey Chirwa akafunga bao Hilo la kusawazisha na kufanya mchezo huo kumalizika Kwa sare hiyo ya bao 1-1.
Kwa matokeo hayo sasa Simba wanarejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakifikisha pointi 16 sawa na Azam na Yanga ila Simba wanakua na faida ya magoli mengi ya kufunga.
No comments