LIGI KUU YA VODACOM : MCHEZO MMOJA TU KUPIGWA LEO JIJINI MWANZA
Baada ya mapumziko ya kupisha kwa ratiba za kalenda ya FIFA Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara inarejea tena wikiend hii ikiwa ni mzunguko wake wa 6 na mechi moja tu ya mzunguko huo ikichezwa leo jioni Jijini mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba baina ya wenyeji Mbao FC dhidi ya Wagonga nyundo wa jiji la Mbeya Klabu ya Mbeya City.
Tayari Mbeya City wako jijini Mwanza ikiwa ni mchezo wao wa kwanza wakiwa na kocha mpya Mburundi
Nsanzurwimo Ramadhani na atakua na kibarua kikubwa dhidi ya Mburundi mwenzie anayeifundisha Mbao FC Ettiene Ndarazigye.
Wenyeji Mbao FC wanakamata nafasi ya 9 katika msimamo wa ligi hiyo mpaka sasa wakiwana pointi zao 5 wakati Mbeya City wao wako katika nafasi ya 7 nwakiwa wameshajikusanyia point 7 huku team zote zikiwa zimecheza michezo mitano.
Michezo mingine ya Ligi hiyo itachezwa kesho Jumamosi na Jumapili ili kukamilisha mzunguko wa 6 kuelekea katika kumpata bingwa mpya wa Ligi yetu kwa msimu huu.

No comments