VALENCIA WA MAN UNITED ASHINDA TUZO YA GOLI BORA LA MWEZI

Man United star Antonio Valencia wins goal of the month
Nahodha msaidizi wa Manchester United na mlinzi wa pembeni wa timu hiyo Antonio Valencia amefanikiwa kushinda tuzo ya goli bora la Mwezi September katika tuzo zinazotolewa kila mwezi kwenye ligi kuu ya Soka nchini England.

Goli la kwanza katika ushindi wa bao 4-0 walioupata Manchester United dhidi ya Everton ndilo lililompa tuzo hiyo akipiga bonge la Shuti nje ya 18 baada ya pasi ya Nemanja Matic.

"nina Furaha kushinda tuzo hii ya goli bora la mwezi na napenda kumshukuru kila mmoja aliyenipigia kura" Alisema valencia

No comments

Powered by Blogger.