WENGER AINGIZWA "CHAKA" HABARI ZA GEORGE WEAH KUSHINDA URAIS NCHINI LIBERIA
![]() |
George Weah akipiga Kura Jumanne wiki hii |
Akiongea na Waandishi wa habari Wenger ambaye alimfundisha George Weah miaka ya 1990 akiwa kocha wa Monaco alisema "Napenda kumpongeza mmoja wa wachezaji wangu wa zamani ambaye ameshinda kiti cha Urais nchini Liberia, Si mara nyingi unakua na mchezaji wako wa zamani anakua Rais wa nchi hivyo nampongeza sana George" alimaliza kusema.
Lakini taarifa toka Nchini Liberia zinasema George Weah hajashinda bado Urais wakati huu kura zikiendelea kuhasabiwa katika Uchaguzi uliofanyika Jumanne wiki hii japokua uwezekano wa George kushinda ni mkubwa kwani anaongoza katika mikoa 11 kati ya 15 ya nchi hiyo ambayo inaingia katika Uchaguzi wa kwanza kupokezana madaraka kwa njia ya amani.
Aliyekua Rais wa nchi hiyo mwanamama Ellen Johnson Sirleaf mwenye miaka 78 amemaliza mihula yake miwili ya Urais akiwa ni rais wa kwanza mwanamke katika bara la Afrika akichaguliwa kwa njia ya kidemokrasia na akitoka kwa njia ya kidemokrasia.
Liberia ni taifa lililozaliwa mnamo karne ya 19 na Watumwa waliokimbia nchini Marekani na kwa miaka 73 limekua moja ya taifa ambalo madaraka yamekua yakirithishwa kwa njia ya bunduki mpaka mwaka 2006 alipoingia Rais Ellen ambaye ameshinda tuzo ya amani ya Nobeli.

George Weah mwenye miaka 51 ambaye ni mwafrika wa kwanza kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Dunia (Balon d'or) anagombea sambamba na mwanamama Jewel Howard Taylor mke wa zamani wa Rais wa nchi hiyo anayetumikia kifungo cha miaka 50 jela Charles Taylor mwanamama huyo atakua makamu wake wa Rais kama atashinda na wanapambana na makamu wa Rais anayemaliza muda wake Joseph Boakai.
No comments