YANGA NA MTIBWA, AZAM NA SINGIDA ZAGAWANA POINTI VPL LEO
Yanga wamezidi kuchechemea katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar, nyumbani katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ulikua wa kuvutia na kwa kiasi fulani Yanga waliutawala wakitengezeza nafasi nyingi za kufunga lakini golikipa wa Mtibwa Sugar Bennedict Tinoco alikua shujaa wa Mtibwa kwa kuokoa michomo mingi iliyoelekezwa langoni kwake kutoka kwa washambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu na Donald Ngoma.
Katika viwanja vingine;
Huko Jamhuri Dodoma Singida United wametoshana nguvu na Azam FC kwa kufungana bao 1-1 sawa na Mbao FC na Tanzania Prisons ambao wamepata sare ya aina hiyo katika uwanja wa CCM Kirumba.
Huko Nangwanda Sijaona Mtwara, wenyeji Ndanda FC wamechomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lipuli FC wakati Ruvu Shooting nao wakiibuka na ushindi kama huo dhidi ya Njombe Mji nyumbani Mabatini.
Huko Mwadui Complex, wenyeji Mwadui FC wametoshana nguvu na Mbeya City kwa kufungana mabao 2-2, Huku Majimaji wakilazimishwa sare ya 0-0 na Kagera Sugar ya Kagera.
Ligi hiyo itaendelea kesho ambapo Stand UTD watawakaribisha Simba katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
No comments