MAN UNITED NA SPURS ZAPIGA 4G LIGI KUU ENGLAND LEO
Manchester United wameendeleza vipigo vya bao 4 katika mechi zake msimu huu wakiifunga Crystal Palace bao 4-0 katika mechi ya ligi kuu ya England kwenye uwanja wa Old Trafford.
United licha ya ushindi huo bado imeendeleza rekodi nzuri ya kutofungwa katika uwanja wake wa nyumbani huku ikiwa imeruhusu mabao mawili tu tangu kuanza kwa msimu huu walipotoka sare ya bao 2-2 na Stoke City ugenini.
Magoli ya United leo yalifungwa na Maruane Fellaini aliyefunga mabao mawili huku Lukaku na Juan Mata wakifunga bao moja kila mmoja.
Katika mechi ya awali leo Tottenham ikiwa ugenini iliweza kushinda bao 4-0 dhidi ya wageni kwenye ligi hiyo Huddersfield town.
Harry Kane alifunga mabao mawili, Ben Davies na Moussa Cissoko walifunga bao moja kila mmoja kukamilisha ushindi huo wa bao 4-0 ugenini.
Katika mechi zingine kwenye ligi hiyo Stoke City wakiwa nyumbani waliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Southampton wakati Leicester City wao waliambulia sare ya bila kufungana na wenyeji AFC Bournemouth
Watford wakiwa ugenini walipata sare ya bao 2-2 dhidi ya wenyeji West Brom kwenye mechi ambayo Watford waliweza kusawazisha bao la pili dakika ya mwisho ya muda wa nyingoza likifungwa na mshambuliaji wake Richalison.
West Ham wakiwa Nyumbani pale London Stadium waliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 bao pekee la dakika za mwisho la mahambuliaji Diafra Sakho.
Mechi inayoendelea hivi sasa ni Chelsea dhidi ya Manchester City katika dimba la Stamford bridge.
No comments