MTIFUANO VPL LEO: YANGA NA MTIBWA,SINGIDA NA AZAM FC, RATIBA YOTE HII HAPA
Mabingwa watetezi Yanga watakua uwanja wa uhuru Dar es Salaam kumenyana na Vinara wa ligi hiyo klabu ya Mtibwa Sugar toka Manungu mkoani Morogoro.
Azam FC ambao nao wako kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo watakua Mkoani Dodoma kucheza na wenyeji Singida United katika dimba la Jamhuri Mkoani humo.
Maji Maji FC watakua katika uwanja wao wa Majimaji mjini Songea kuwakaribisha Kagera Sugar ambao msimu huu wameuanza vibaya.
Wachimba Madini wa Mwadui klabu ya Mwadui FC wao watakua Mwadui Complex kuwakaribisha wagonga nyundo wa jiji la Mbeya klabu ya Mbeya City.
Mbao FC baada ya kutoka sare na Simba watabaki Jijini Mwanza kuwakaribisha Tanzania Prisons kutoka Mbeya pambano litakalochezwa kwenye dimba la
CCM Kirumba.
Ndanda FC watakua katika uwanja wao wa nyumbani kucheza dhidi ya Lipuli FC kutoka Iringa huku Ruvu Shooting wakicheza na Njombe Mji katika dimba la Mabatini pale Pale Kibaha.
Kesho utachezwa mchezo mmoja tu kati ya Stand United na Simba kwenye dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga.
No comments