UBORA WA LUKAKU UMETOKANA NA UBORA WA TIMU - MOURINHO
Akiwa ameshafunga magoli 10 katika mechi 9 za mashindano yote msimu huu, Romelu Lukaku ameendelea kuwa mwiba mkali kwa nyavu za timu pinzani.
"Anafanya kazi nzuri sana, ni mafanikio mazuri kwake, lakini haya yote yanawezekana kama ukiwa na timu nzuri. Bila timu nzuri huwezi kufanya haya, kwa sasa timu inacheza vizuri sana, kuna rekodi nzuri sana kwa Lukaku, na atafanya mengi zaidi kwani anapenda kujifunza na kufanya vizuri zaidi" Mourinho akimzungumzia Lukaku.
Akizungumzia ushindi wa goli 4 dhidi ya CSKA Moscow Mourinho alisema "Ulikuwa ni ushindi mzuri kwetu, kupata pointi sita katika mechi za ligi ya mabingwa Ulaya ni jambo zuri kwa timu na linatuongezea kujiamini, Lakini hili pia ni zuri kwa mchezaji mwenyewe."
Mourinho aliamua pia kuwapa kongole wachezaji wake amabo hawakuweza kuanza katika mechi za nyuma lakini jana walipewa nafasi na kufanya vizuri, alisema Smalling na Lindelof wamecheza vizuri sana, Herera pamoja na kutoanza katika mechi nyingi lakini alikuwa na mchezo mzuri sana, na Martial pia alikuwa na mchezo mzuri"
Kocha huyo mwenye maneno mengi hakuwaacha salama chama cha soka cha England (FA) kuhusu upangaji ratiba. Mourinho akawatupia dongo kwa kusema "Unapozungumzia Ligi kuu England Unazungumzia habari nyingine, tunatakiwa kucheza saa 11 jioni Jumamosi dhidi ya Crystal Palace, wakati huo umetoka kucheza jumatano usiku huku Moscow ukiangalia Liverpool anamapumzika marefu kuliko sisi, akiwa amecheza hapa hapa Moscow jumanne lakini atacheza jumapili"
"Tumeenza msimu vizuri sana mwezi August na September, na sasa tumebakisha mechi moja ngumu, kikubwa ni kuendelea kufanya juhudi na kutokata tamaa, akili zetu zote kuzielekeza kwenye michezo yetu na tutafanikiwa kwa sababu bado tuna msimu mzuri sana kwetu." Alimaliza Kocha huyo mwenye mbwembwe na maneno
No comments