REAL MADRID NA ATLETICO MADRID ZABANWA MBAVU LA LIGA
Mafahari wawili wa jiji la Madrid nchini Spain klabu za Real Madrid ambao ni mabingwa watetezi wa La Liga pamoja na Atletico Madrid wamekutana na ugumu kwenye mechi zao za leo La Liga.
Real Madrid ikiwa nyumbani Santiago Bernabeu ilijikuta ikilazimishwa sare ya bao 1-1 na Levante huku Levante wakitangulia kupata bao dakika ya 12 ya mchezo likifungwa na Ivi Lopez kabla ya Lucas Vasquez hajaisawazishia Real Madrid bao dakika ya 36 magoli ambayo yalidumu mpaka mwisho wa mchezo.
Katika mchezo huo Marcelo alionyeshwa kadi nyekundu baada ya mchezo usio wa kiungwana
Atletico Madrid wao wakiwa ugenini walienda sare tasa na Wenyeji wao Valencia mchezo uliokua mkali na wenye kosakosa nyingi dakika zote 90.
Mechi inayoendelea wakati huu ni Sevilla dhidi ya Eibar wakati Barcelona wataialika Espanyol badae.

No comments