ARSENAL, TOTTENHAM NA CHELSEA ZAGAWA DOZI LIGI KUU ENGLAND


Ukiacha mchezo wa awali baina ya Wenyeji Manchester City dhidi ya Liverpool ambapo Manchester City iliibuka na ushindi mnono wa bao 5-0 mechi zingine 5 zilichezwa katika hatua ya 4 ya ligi kuu ya England msimu huu

Arsenal wakiwa nyumbani waliweza kuibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya AFC BOURNEMOUTH  mchezo uliopigwa katika dimba la Emirates Jijini London.

Danny Welbeck alifunga bao 2 peke yake huku mshambuliaji mpya wa Arsenal Alexandre Lacazette akifunga bao moja.

Chelsea ambao ni mabingwa wa ligi hiyo walisafiri mpaka katika uwanja wa King power KUIVAA Leicester City na Chelsea kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 Magoli ya Alvaro Morata na Ng'olo Kante huku Jermie Vardy akifunga bao pekee la Leicester City.

Everton ikiwa nyumbani ilikumbana na kichapo cha bao 3-0 toka kwa Tottenham Hotspur magoli ya Harry Kane aliyefunga mabao mawili huku Christian Eriksen akufunga bao moja.

Southampton wakiwa nyumbani wakafungwa bao 2-0 toka kwa Watford huku Brighton & Hoev wakiishangaza West Bromwich Albion kwa kuifunga bao 3-1

Mechi ya mwisho leo ni baina ya Stoke City vs Manchester United

No comments

Powered by Blogger.